Profesa Assad afunguka
Dar es Salaam. Hatimaye Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amefunguka kuhusu baadhi ya tuhuma dhidi yake kuwa alilidharau Bunge baada ya kutumia neno “udhaifu” katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Profesa Assad amesema anashutumiwa bila ya makosa na kwamba anaichukulia hatua hiyo ya Bunge kwa utulivu na suala hilo halimsumbui. Bunge lilifikia azimio la kutoshirikiana na Profesa Assad mapema wiki hii baada ya kumkuta na hatia ya kusema “udhaifu wa Bunge” wakati alipohojiwa kuhusu kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo huibua ufisadi, kutofuatwa kwa kanuni za fedha, kasoro zinazosababisha kuwepo na wafanyakazi hewa na nyingine za kiutendaji. CAG Assad, ambaye kwa kawaida si mzungumzaji wa mara kwa mara na vyombo vya habari, jana alikubali kutoa muda wake kuzungumzia sakata hilo. Aliiambia gazeti la The Citizen linalochapishwa na Mwananchi Communications Limited (MCL), ...