Askari ‘wapita pita’ mitaani Moshi




Makundi ya askari wakiwa wamebeba silaha, yameonekana leo asubuhi katika maeneo mbalimbali mjini Moshi.
MCL Digital, ilipita maeneo mbalimbali ikiwamo Soko la Mbuyuni, Manyema pamoja na soko la kati huku watu wakiendelea na shughuli zao.
Akizungumza na Mcl Digital Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah amesema hali iko shwari.
 Awali, kulikuwapo na tishio la maandamano leo katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.


Comments

Popular Posts