Shangazi aulizia dola 300milioni za makinikia
Mbunge wa Mlalo (CCM) Rashid Shangazi
Dodoma. Mbunge wa Mlalo (CCM) Rashid Shangazi amemtaka Waziri wa Madini, Angellah Kairuki kutoa ufafanuzi wa dola milioni 300 za makinikia.
Shangazi akichangia bajeti ya wizara ya madini ya mwaka 2018/19 leo bungeni Mei 31, 2018 amesema ufafanuzi huo utahitimisha sintofahamu iliyopo.
"Nimesoma kitabu (cha hotuba ya bajeti), sijaona zile dola 300 za Makinikia ziko wapi. Natambua Profesa (Palamagamba) Kabudi alikuwa anashughulikia."
Shangazi ameongeza; “ni vyema tungepata majibu ili kuondoa sintofahamu ya jambo hilo."
Makinikia
Dola 300 milioni ni zile zilizobainishwa na taarifa ya kamati ya kuchunguza mchanga wa madini (makinikia) kuwa Usd 20 bilioni zimeibwa na Acacia.
Lakini TRA wakaongeza na riba na adhabu ya kuchelewa kulipa ikafikia usd 190 bilioni.
Baada ya majadiliano, Barick Gold walikubali kulipa usd 300 milioni ya Usd 190 bilioni.
Comments
Post a Comment