Wazazi wa wanafunzi St Florence waanza kuhamisha watoto
Dar es Salaam. Baadhi ya wazazi wameanza kufuatilia uhamisho wa watoto wao baada ya kusambaa kwa taarifa zinazodai mwalimu wa kiume katika Shule ya St Florence jijini Dar es Salaam anawanajisi wanafunzi.
Tangu jana jioni kumekuwa na taarifa za mwalimu mmoja wa shule hiyo kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba, jambo lililozua taharuki.
leo, Machi 31, 2018 wazazi hao wakihangaikia uhamisho huku wale wenye watoto wa darasa la saba wakishindwa kufanya hivyo.
"Tangu nipate taarifa hizi sijapata usingizi kulipokucha tu nimekuja kumuondoa mwanangu wa darasa la nne, hii hali inatisha," amesema mzazi mmoja aliyejitambulusha kwa jina moja na Aneth.
Mzazi mwingine alisema hajafanikiwa kupata uhamisho wa watoto wake wa darasa la saba, lakini hatamuacha aendelee kukaa shuleni hapo.
zaidi ya wazazi kumi wakihangaikia uhamisho wa watoto wao japo bado uongozi wa shule haujazungumza chochote.
Comments
Post a Comment