Spika: Kuzungumza na Waziri Mkuu dakika moja tu
Waziri Mkuu, Kassim Majiliwa akimweleza jambo Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege wakati bunge lilipokuwa likijadili Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, jijini Dodoma jana.
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka wabunge kutumia dakika moja kuzungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na si vinginevyo.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo jana jioni bungeni Juni 19, 2018 baada ya wabunge kuwa wanakwenda mara kwa mara eneo alilokaa na kuzungumza naye.
“Niwaombe mnaokwenda kwa Waziri Mkuu (Majaliwa) mkae dakika moja, Waziri Mkuu lazima asikie kinachoendelea humu,” amesema Spika Ndugai
Naye mbunge wa Hanang’ (CCM), Dk Mary Nagu akichangia bajeti ya serikali ameipongeza kwa kusema ni nzuri huku akimwomba Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuitekeleza ili kuleta ustawi wa jamii.
Amesema kuondoa kodi ya taulo za kike ni kujali jamii na akaiomba wizara ya afya na ile ya viwanda na biashara kuhakikisha wanaonufaika ni watumiaji na si waagizaji.
Amesema viwanda vinavyojengwa haviwalengi wananchi au halmashauri, “kwani kila kiwanda kinachojengwa, tozo zote zinachukuliwa na Serikali, kungekuwa na mgawanyiko, kwamba viwanda vikubwa vitozwe na Serikali na vidogo vichukuliwe na halmashauri.”
Comments
Post a Comment